WAD 2021
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani kitaifa
yamefanyika mkoani Mbeya tarehe 1 Desemba 2021. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa. Maadhimisho yalianza
tarehe 24/11/2021 kwa matembezi ya hisani ya kuchangia mfuko wa Udhamini wa
kudhibiti UKIMWI ambapo mgeni rasmi aliku naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk.
Tulia Akson na maonyesho ya shughuli mbali mbali za VVU na UKIMWI ziliendelea
ikiwa nipamoja na kutolewa huduma za afya kama vile kupima VVU, saratani ya
mlango wa kizazi, Tohara kwa Wanaume pamoja na chanjo ya COVID
Kauli Mbiu ya Maadhimisho haya ilikuwa ni "ZINGATIA USAWA, TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO"