News

Find what's going on with us

STEPS TANZANIA YAKABIDHI ZANA ZA KAZI KWA WAELIMISHA RIKA NGAZI YA JAMII KUPITIA MRADI WA GLOBAL FUND C7

STEPS Tanzania kupitia Ofisi ya Kanda ya Mashariki imekabidhi Zana za kufanyia kazi kwa Waelimishaji Rika ngazi ya jamii (Peer Educators) wanaotekeleza Mradi wa Global Fund C7 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Zoezi hili ni sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa shughuli za kijamii na afya katika jamii kwa kuhakikisha waelimishaji rika wanapata vitendea kazi muhimu vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mpango huu utaendelea pia katika mikoa ya Morogoro na Tanga kwa upande wa Kanda ya Mashariki, huku Kanda ya Kusini ikihusisha mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma ambayo nayo itanufaika na vitendea kazi hivyo.

Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni vitambulisho, mabegi pamoja na kofia maalum kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi.

STEPS Tanzania inaendelea kutoa shukrani za dhati kwa CSSC na NASHCoP kwa maandalizi na uratibu wa zana hizo, pamoja na Global Fund C7 kwa kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi hivyo kupitia ufadhili wao.

Aidha, tunawapongeza Waelimishaji Rika wote kwa hatua hii muhimu na kuwahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uwajibikaji huku wakivitunza vizuri vitendea kazi walivyokabidhiwa kwa manufaa ya jamii wanayoihudumia.