News

Find what's going on with us

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Watembelea na Kukagua Maendeleo ya Mradi wa TUENDELEE PAMOJA katika Wilaya ya Kisarawe.

Mwakilishi toka Ubalozi wa Marekani Bi. Stella Mtega ameambatana na STEPS Tanzania katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa #tuendeleepamojaproject . Mradi huo unatekelezwa na STEPS Tanzania katika kata za Masaki, Msanga, Kisarawe na Mzenga za Wilaya ya Kisarawe kwa ufadhili toka Mfuko wa Balozi wa Marekani. Mradi huo unalenga kuwezesha kiuchumi WAVIU kupitia vikudi vilivyo chini ya Konga. Katika ziara hiyo, Mwakilishi toka Ubalozi wa Marekani na STEPS Tanzania walipata  fursa ya kukutana na viongozi wa Konga ya WAVIU wanaonufaika na mradi, wawakilishi wa serikali kupitia wilaya ya Kisalawe, na washiriki wa jamii (WAVIU) wanaonufaika na mradi huo.

katika Picha Ni Afisa Msimamizi wa ruzuku wa Mfuko AFHR  toka Ubalozi wa Marekani Bi Stella akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe,Mratibu wa shughuli za UKIMWI wa Halmashauri (CHAC) wa Kisarawe,  Mkurugenzi toka STEPS Tanzania pamoja na Uongozi wa Konga ya Kisarawe walipokuwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe.

Lengo kuu lilikuwa kupata ufahamu wa kina kuhusu utekelezaji wa mradi, mafanikio yaliyopatikana hadi sasa, na changamoto zinazowakabili washiriki katika kutekeleza mradi huo.Wakati wa ziara, maendeleo chanya yamebainika kufanywa na mradi wa Tuendelee Pamoja. Baadhi ya mafanikio ni pamoja na uanzishwaji wa shughuli za ufugaji wa Kuku wa kienyeji kwa Kila Mwanakikundi,HISA kwa Wanakikundi, mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha, na ushirikishwaji wa WAVIU katika huduma za afya kwa watu wanaoishi na VVU.


Hata hivyo, Ubalozi wa Marekani na timu ya STEPS Tanzania iligundua baadhi ya changamoto ambazo ni pamoja na upatikanaji mdogo wa mitaji ya kutosha,uhaba wa watendaji wa kutosha katika kata ambao wanatoa huduma za mifugo,umbali kwa baadhi ya wanakikundi hivyo kupelekea kukosa kushiriki vikao, Pamoja na magonjwa yanayokabili kuku wanaowafuga ambao baadhi imepelekea kuku hao kufa.STEPS Tanzania ilitoa mapendekezo kwa wadau wote waliohusika ktk utekelezaji wa mradi ambayo ni kuendelea kuimarisha upatikanaji wa mitaji, kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu mradi, na kuboresha upatikanaji wa huduma kwenye mifugo hususani kuku kutoka kwa bwana afya wa kata zao.



Ziara ya Ubalozi wa Marekani na STEPS Tanzania ilihitimishwa kwa kujenga ushirikiano na wadau wa mradi na kuzihimiza pande zote kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha malengo ya mradi. @usembassytz @pepfar @tacaidsinfo @nacophatz