Steps Tanzania yatoa mafunzo kwa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (CHW) juu ya kutoa huduma na kupambana na Magonjwa ya UVIKO 19 na Kifua Kikuu.
Katika kutekeleza
Mradi wa C19RM unaofadhiliwa na Global Fund Kupitia kwa Amref Health Africa in
Tanzania @amreftz , Steps Tanzania imetekeleza afunzo hayo kwa Wahudumu wa Afya
Ngazi ya Jamii (CHW) katika Wilaya za Bariadi CC, Bariadi DC, Maswa , Busega,
Meatu na Itilima za Mkoa wa Simiyu huku Dodoma CC, Chamwino na Chemba kwa Mkoa
wa Dodoma.
Mafunzo hayo
yaliwawezesha CHW kutambua uhusiano na tofauti zilizopo kati ya magonjwa ya
UVIKO 19 na TB pamoja na kujua njia mbali mbali za kuenea kwake ambazo kwa
asilimia kubwa hufanana.
Pia waliweza kujengewa
uwezo juu ya mbinu/ namna mbalimbali za kutatua changamoto zinazoibuka katika
jamii kipindi wanapofanya uhamasishaji na utoaji wa elimu juu ya chanjo ya
UVIKO 19.